
Madereva wametangaza kumaliza mgomo baada ya kufikia muafaka na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na kuundwa kwa kamati itakayosimamia matatizo ya madereva na kutoa taarifa baada ya siku saba. Mabasi ya mikoani kutoka Ubungo sasa yameanza safari baada ya mgomo wa takriban siku 2. Makubaliano yaliyofikiwa ni kuundwa kwa kamati ya madereva zaidi ya 8 watakaokutana na mkuu wa wilaya kuanzia kesho. Kamati iliyoundwa inatakiwa kujadili madai yao kwa muda usiozidi siku 7 kwa usimamizi wa Mkuu wa Wilaya Paul Makonda.
No comments:
Post a Comment