WAGOMBEA URAIS WAIBUA MPASUKO KWA WASANII WA TANZANIA


“Mastaa wamegawanyika. Wale waliopata bahati ya kwenda kama kina Dully Sykes, Tunda Man, Khadija Kopa, Nay wa Mitego wameibua minong’ono kwamba kuna fitina wamefanya ili wenzao wakose nafasi hiyo waneemeke peke yao. Waliokosa nafasi nao wamejiunga na kuanza kutafuta kambi kwa mgombea mwingine,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, mastaa kama Judith Wambura ‘Jide’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Steven ‘JB’ wao walifanya fitina kivyao na kufanikiwa kuinasa kambi ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wasira ambaye alitangaza nia ya kuwania urais Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Mwanza.

Wasanii hao walipopigiwa simu na kuulizwa kuhusiana na mpasuko huo, walidai hawaoni kama ni tatizo kutofautiana kwa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu kwani ndiyo siasa ilivyo.
“Wewe acha tutofautiane kisiasa lakini zikipita tunarudi kwenye mstari mmoja kwani mashabiki wetu ukishapita uchaguzi wanasahau,” alisema mmoja wa wasanii hao aliyeomba hifadhi ya jina.
No comments:
Post a Comment