UTUKUFUHUU BLOG KAMA ILIVYO KAWAIDA YETU TUNAKUTANGAZIA KUWA HIVI PUNDE TUTAANZA KUANGALIZIA MAJINA YA WALIOPATA MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016 KUTOKA BODI YA MKOPO PUNDE TU BAADA YA MAJINA KUKAMILISHWA UTAKUWA UKITUMA JINA LAKO eg THOMAS-JUMA(MKOPO) TO 0768248512/0673796095 asante na karibu
bofya hapa ujionee
Saturday, 9 May 2015
NANI KUWA MWANASOKA BORA KWA WANAWAKE DUNIANI KATI YA HAWA
Mashabiki wanapewa fursa kumpigia
kura mchezaji bora wa soka wa BBC mwaka huu kwa upande wa wanawake
likiwa ni taji la kwanza kuandaliwa na chombo cha habari cha
kimataifa.Taji hilo litawasheherekea wachezaji wenye mchezo wa juu
wanaoshindana katika mchezo unaoimarika kwa kasi duniani.Jopo la
wataalam wakiwemo wasimamisi,waandishi,makocha na wachezaji wa zamani
wanashirikiana kumtafuta mcheza huyo miongoni mwa wachezaji watano
walioteuliwa.Wanaogombania taji hilo watatangazwa mnamo tarehe 26 mwezi
Aprili huku mshindi akitangazwa mnamo mwezi May.''Tuzo hilo ni fursa
muhimu kuangazia viwango vya mchezo na vipaji vilivyopo katika soka ya
wanawake duniani,'' alisema Caroline Rigby,muhariri mkuu wa taji la BBC
la mchezaji bora wa soka ya wanawake mwaka huu duniani. Taji hilo la BBC
lilizinduliwa kabla ya michuano ya kombe la dunia upande wa wanawake
itakayofanyika nchini Canada mwezi Juni.
Veronica
Veronica Boquete (Spain and Frankfurt)
Kiungo wa kati huyo mwenye miaka 27 alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya
Uhispania iliofuzu katika dimba la kombe la dunia kwa mara ya
kwanza.Akiwa mwenye kipaji cha kufunga mabao amefunga mabao 29 kati ya
mechi 42 alizocheza.Pia anajulikana kama mwanamke ambaye mwaka 2013
alianza kampeni ya kuwashirikisha wachezaji wa kike katika msururu wa
mechi za FIFA za kutoa faraja alipopata sahihi 20,000 .Amesema kuwa
:''Ninafurahi kuteuliwa katika orodha ya taji la mchezaji bora wa soka
upande wa wanawake duniani.Hii inamaanisha kuwa nimekuwa nikifanya kazi
nzuri miaka iliopita.pia inanipa motosha katika siku zijazo''.
Marta
Marta (Brazil and FC Rosengard)
Marta anadaiwa kuwa maarufu katika soka ya wanawake duniani.akiwa na
umri wa miaka 29,mshambuliaji huyo wa kikosi cha Brazil amefunga bao
moja katika kila mechi ya kimataifa aliyocheza akionekana kuwa juu ya
kipawa chake.Baada ya kushinda ligi ya nyumbani mwaka 2014 nchini Sweden
kwa mara ya sita,alishindwa katika fainali ya kilabu bingwa Ulaya
upande wa akina dada-lakini Marta alishinda taji la ligi kuu nchini
Sweden Svenska mwaka huu. Anasema kuwa:''nafurahi sana kwa
kuteuliwa.Tayari najihisi mshindi kwa kuorodheshwa katika fainali ya
wachezaji watano.Ni muhimu kwa kuwa unahukumiwa na mashabiki wa
soka,wale wanaokufuata''.
Kim Little
Kim Little (Scotland and Seattle Reign)
Mchezaji Scotland Little amekuwa na msimu mzuri katika ligi ya soka ya
wanawake nchini Marekani ambapo anacheza kama mshambuliaji wa kiungo cha
kati.Scotland aliongoza kwa mabao 16 mbali na kuchaguliwa kama mchezaji
bora wa mwezi mara tatu mbali na kutajwa kuwa mchezaji bora katika
msimu ambao timu yake Seattle,ilifuzu katika fainali kabla ya kupoteza
mechi hiyo kwa kilabu ya Kansas.Ijapokuwa ana miaka 24,amecheza katika
michuano ya kulipwa tangu mwaka 2006 na mwaka 2013 alichaguliwa kama
mchezaji bora wa taji la PFA.Hatahivyo anaendelea kujiliwaza baada ya
Scotland kushindwa kufaula kwa dimba la duniani nchini Canada
2015.Anasema:''Kufuatia kuwepo kwa wachezaji bora duniani na katika ligi
ya Marekani kwangu mimi ni heshima kubwa kutambulika''.
KesslerNadine Kessler (Germany and Wolfsburg)
Ni nahodha wa timu bora barani Ulaya mbali na kuwa tegemeo la timu ya
taifa ya Ujerumani, hakuna taji lolote katika soka ya wanawake ambalo
Kessler hajashinda.Mchezaji huyo wa miaka 27 aliiongoza klabu ya
Ujerumani Wolfsburg kushinda taji lao la pili la ligi ya wanawake barani
Ulaya UEFA pamoja na taji la ligi ya Bundesliga msimu uliopita.Yote
haya yalimwezesha kupata taji la FIFA la mchezaji bora wa mwaka 2015
duniani upande wa akina dada na kumrithi mchezaji mwenza wa Ujerumani
Nadine Angerer.Hatahivyo kuna maswali mengi kuhusu iwapo majeraha mengi
aliyonayo yatamruhusu kung'ara katika dimba la Canada mwaka
huu.Anasema:''nilitaka kucheza soka ili kufanikiwa.lakini sidhani kwamba
kitu kama hiki kinaweza kufanyika''.
Oshoala
Asisat Oshoala (Nigeria and Liverpool)
Chipukizi Asisat Oshoala ni mchezaji wa kwanza kutoka Africa kushindana
katika ligi ya soka ya wanawake.Akiwa na mataji ya mchezaji bora wa
mwaka na mchezaji bora chipukizi mwaka huu,alijiunga na mabingwa wa ligi
Liverpool kutoka Rivers Angels.Kwa jina la utani Seedorf,alikuwa
mchezaji bora wa mchuano wa kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20
pamoja na kuisadia Nigeria kufuzu katika kombe la dunia nchini
Canada.Vilevile alituzwa na rais wa Nigeria .Anasema:''Nahisi
kukubalika. Niliweka juhudi kubwa mwaka uliopita lakini nimeshangazwa na
uteuzi huu.Tuzo hii ni kitu kizuri sana katika soka ya wanawake,
inaweza kutusaidia kwa kutoa motisha kwa mataifa mengine kuwasaidia
wanawake wao na kuwachukulia sawa tu na wanaume''.
No comments:
Post a Comment