Mashabiki wanapewa fursa kumpigia
kura mchezaji bora wa soka wa BBC mwaka huu kwa upande wa wanawake
likiwa ni taji la kwanza kuandaliwa na chombo cha habari cha
kimataifa.Taji hilo litawasheherekea wachezaji wenye mchezo wa juu
wanaoshindana katika mchezo unaoimarika kwa kasi duniani.Jopo la
wataalam wakiwemo wasimamisi,waandishi,makocha na wachezaji wa zamani
wanashirikiana kumtafuta mcheza huyo miongoni mwa wachezaji watano
walioteuliwa.Wanaogombania taji hilo watatangazwa mnamo tarehe 26 mwezi
Aprili huku mshindi akitangazwa mnamo mwezi May.''Tuzo hilo ni fursa
muhimu kuangazia viwango vya mchezo na vipaji vilivyopo katika soka ya
wanawake duniani,'' alisema Caroline Rigby,muhariri mkuu wa taji la BBC
la mchezaji bora wa soka ya wanawake mwaka huu duniani. Taji hilo la BBC
lilizinduliwa kabla ya michuano ya kombe la dunia upande wa wanawake
itakayofanyika nchini Canada mwezi Juni.
Veronica Boquete (Spain and Frankfurt)
Kiungo wa kati huyo mwenye miaka 27 alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya
Uhispania iliofuzu katika dimba la kombe la dunia kwa mara ya
kwanza.Akiwa mwenye kipaji cha kufunga mabao amefunga mabao 29 kati ya
mechi 42 alizocheza.Pia anajulikana kama mwanamke ambaye mwaka 2013
alianza kampeni ya kuwashirikisha wachezaji wa kike katika msururu wa
mechi za FIFA za kutoa faraja alipopata sahihi 20,000 .Amesema kuwa
:''Ninafurahi kuteuliwa katika orodha ya taji la mchezaji bora wa soka
upande wa wanawake duniani.Hii inamaanisha kuwa nimekuwa nikifanya kazi
nzuri miaka iliopita.pia inanipa motosha katika siku zijazo''.Marta (Brazil and FC Rosengard) Marta anadaiwa kuwa maarufu katika soka ya wanawake duniani.akiwa na umri wa miaka 29,mshambuliaji huyo wa kikosi cha Brazil amefunga bao moja katika kila mechi ya kimataifa aliyocheza akionekana kuwa juu ya kipawa chake.Baada ya kushinda ligi ya nyumbani mwaka 2014 nchini Sweden kwa mara ya sita,alishindwa katika fainali ya kilabu bingwa Ulaya upande wa akina dada-lakini Marta alishinda taji la ligi kuu nchini Sweden Svenska mwaka huu. Anasema kuwa:''nafurahi sana kwa kuteuliwa.Tayari najihisi mshindi kwa kuorodheshwa katika fainali ya wachezaji watano.Ni muhimu kwa kuwa unahukumiwa na mashabiki wa soka,wale wanaokufuata''.
Kim Little (Scotland and Seattle Reign) Mchezaji Scotland Little amekuwa na msimu mzuri katika ligi ya soka ya wanawake nchini Marekani ambapo anacheza kama mshambuliaji wa kiungo cha kati.Scotland aliongoza kwa mabao 16 mbali na kuchaguliwa kama
mchezaji bora wa mwezi mara tatu mbali na kutajwa kuwa mchezaji bora katika msimu ambao timu yake Seattle,ilifuzu katika fainali kabla ya kupoteza mechi hiyo kwa kilabu ya Kansas.Ijapokuwa ana miaka 24,amecheza katika michuano ya kulipwa tangu mwaka 2006 na mwaka 2013 alichaguliwa kama mchezaji bora wa taji la PFA.Hatahivyo anaendelea kujiliwaza baada ya Scotland kushindwa kufaula kwa dimba la duniani nchini Canada 2015.Anasema:''Kufuatia kuwepo kwa wachezaji bora duniani na katika ligi ya Marekani kwangu mimi ni heshima kubwa kutambulika''.
Nadine Kessler (Germany and Wolfsburg) Ni nahodha wa timu bora barani Ulaya mbali na kuwa tegemeo la timu ya taifa ya Ujerumani, hakuna taji lolote katika soka ya wanawake ambalo Kessler hajashinda.Mchezaji huyo wa miaka 27 aliiongoza klabu ya Ujerumani Wolfsburg kushinda taji lao la pili la ligi ya wanawake barani Ulaya UEFA pamoja na taji la ligi ya Bundesliga msimu uliopita.Yote haya yalimwezesha kupata taji la FIFA la mchezaji bora wa mwaka 2015 duniani upande wa akina dada na kumrithi mchezaji mwenza wa Ujerumani Nadine Angerer.Hatahivyo kuna maswali mengi kuhusu iwapo majeraha mengi aliyonayo yatamruhusu kung'ara katika dimba la Canada mwaka huu.Anasema:''nilitaka kucheza soka ili kufanikiwa.lakini sidhani kwamba kitu kama hiki kinaweza kufanyika''.
Asisat Oshoala (Nigeria and Liverpool) Chipukizi Asisat Oshoala ni mchezaji wa kwanza kutoka Africa kushindana katika ligi ya soka ya wanawake.Akiwa na mataji ya mchezaji bora wa mwaka na mchezaji bora chipukizi mwaka huu,alijiunga na mabingwa wa ligi Liverpool kutoka Rivers Angels.Kwa jina la utani Seedorf,alikuwa mchezaji bora wa mchuano wa kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20 pamoja na kuisadia Nigeria kufuzu katika kombe la dunia nchini Canada.Vilevile alituzwa na rais wa Nigeria .Anasema:''Nahisi kukubalika. Niliweka juhudi kubwa mwaka uliopita lakini nimeshangazwa na uteuzi huu.Tuzo hii ni kitu kizuri sana katika soka ya wanawake, inaweza kutusaidia kwa kutoa motisha kwa mataifa mengine kuwasaidia wanawake wao na kuwachukulia sawa tu na wanaume''.
No comments:
Post a Comment