LUGOYE THOMAS-the only one.UTUKUFUHUU.BLOGSPOT.COM
KUNDI la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo
tarehe 25 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni.
Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast
Jet.
Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo
na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati
Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata
taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya
Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa…
KUNDI
la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 25
Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi
hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast
Jet.
Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo
na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati
Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata
taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya
Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika
kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya
kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015
No comments:
Post a Comment