MPYA:"CHADEMA(Ukawa) NOMA SANA!! WAFANYA MAAJABU SHINYANGA MJINI,MGOMBEA WA UBUNGE APATIKANA!!"
|
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(BAVICHA) taifa Patrobas Katambi akizungumza katika mkutano huo ambapo alitangaza rasmi nia kugombea ubunge wa jimbo la
Shinyanga Mjini Kupitia UKAWA katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Katambi alisema yeye ni mzaliwa wa Shinyanga hivyo atakomaa katika jimbo la Shinyanga
Mjini kuhakikisha anagombea ubunge ili kuondoa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi
ambao umekuwa ukifanya ubadhirifu wa fedha na kutowaletea maendeleo wananchi.
|
“Mimi
ni mtu wa Shinyanga,Natangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika jimbo
la Shinyanga Mjini,uwezo ninao na nia ninayo,naungana na watangaza nia
wengine waliotangulia,naomba ushirikiano tu,kama jina langu litapitishwa
tutafanya mambo makubwa katika jimbo hili”,alieleza Katambi.
|
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la mkutano.“Sijajipitisha kugombea,bali nitafuata taratibu za Chama
change,nitaandika barua kupeleka jina langu ili kusimikwa kuwa mgombea wa
ubunge na endapo atapitishwa mtu mwingine zaidi yangu,tutamuunga mkono kwani
chama chetu ni cha Umoja na tunafanya kazi moja ya kuleta ukombozi kwa
wananchi”,alieleza Katambi.
|
|
Kushoto
ni Mtangaza nia ya Ubunge Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akiwa na
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambaye naye alijigamba kuwania
ubunge katika jimbo lake.
Wakazi
wa Shinyanga wakifurahia baada ya kusikia kuwa Bwana Patrobas Katambi
kuwa atawania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini ambalo sasa
linaongozwa na mbunge wa CCM ndugu Stephen Masele |
|
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amewataka
watanzania Kumpuuza kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kwa madai
kuwa amepewa pesa na CCM ili azunguke nchi nzima kuvuruga Chadema(UKAWA) lakini
akasisitiza kuwa Kamwe Hataweza kwani wameshajua anachokifanya ndiyo maana
kwenye mikutano yake hathubutu kuisema vibaya CHADEMA na maeneo aliyothubutu
wananchi wamekuwa wakimzomea. |
|
Godbless
Lema pia alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kufanya kazi kwa
kuzingatia sheria za nchi badala ya kupendelea chama Tawala. |
|
Mbunge
Lema pia alisema Kitendo cha Zitto Kabwe kujitangaza kuwa ni Mzalendo
ni Unafiki Mtupu kwani Uzalendo haupimwi kwa Umaskini kwani hakuna mtu
anayependa kuwa maskini kila mtu anapenda kuwa na maisha mazuri. |
|
Mkutano
unaendelea-Lema pia alidai kuwa Matatizo mengi yaliyopo nchini Tanzania
siyo CCM bali ni Uoga wa Watanzania wenyewe kufanya maamuzi magumu |
|
Jukwaa kuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano |
|
Mkutano unaendelea |
|
Jukwaa kuu wakifuatilia hotuba ya mheshimiwa Godbless Lema |
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano |
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde blog
Kabwe Zuberi Zitto (born 24 September 1976), popularly known as Zitto
Kabwe, is a Tanzanian politician.He was a member of the opposition
party, Chadema, from 1992 until his expulsion in March 2015. He served
as a Member of Parliament for the Kigoma North constituency from 2005 to
2015.On 20 March 2015, he officially joined the Alliance for Change and
Transparency.
No comments:
Post a Comment