WAGOMBEA URAIS WAIBUA MPASUKO KWA WASANII WA TANZANIA
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mastaa hao, mpasuko
umejidhihirisha hadharani Jumamosi iliyopita baada ya baadhi ya mastaa
kupata shavu la kwenda kutumbuiza katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Kiluta wakati Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa
alipokuwa akitangaza nia.“Mastaa wamegawanyika. Wale waliopata bahati ya kwenda kama kina Dully Sykes, Tunda Man, Khadija Kopa, Nay wa Mitego wameibua minong’ono kwamba kuna fitina wamefanya ili wenzao wakose nafasi hiyo waneemeke peke yao. Waliokosa nafasi nao wamejiunga na kuanza kutafuta kambi kwa mgombea mwingine,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, mastaa kama Judith Wambura ‘Jide’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Steven ‘JB’ wao walifanya fitina kivyao na kufanikiwa kuinasa kambi ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wasira ambaye alitangaza nia ya kuwania urais Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Mwanza.
“Wamefanya fitina zao wakafanikiwa kupata shavu la Wasira, hapo unaambiwa nao wanahakikisha hakuna msanii anayeongezeka kwenye kambi yao ili waendelee kula fedha zao, yaani ni rafu kwelikweli,” kilisema chanzo.
Wasanii hao walipopigiwa simu na kuulizwa kuhusiana na mpasuko huo, walidai hawaoni kama ni tatizo kutofautiana kwa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu kwani ndiyo siasa ilivyo.
“Wewe acha tutofautiane kisiasa lakini zikipita tunarudi kwenye mstari mmoja kwani mashabiki wetu ukishapita uchaguzi wanasahau,” alisema mmoja wa wasanii hao aliyeomba hifadhi ya jina.
No comments:
Post a Comment