UTUKUFUHUU BLOG KAMA ILIVYO KAWAIDA YETU TUNAKUTANGAZIA KUWA HIVI PUNDE TUTAANZA KUANGALIZIA MAJINA YA WALIOPATA MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016 KUTOKA BODI YA MKOPO PUNDE TU BAADA YA MAJINA KUKAMILISHWA UTAKUWA UKITUMA JINA LAKO eg THOMAS-JUMA(MKOPO) TO 0768248512/0673796095 asante na karibu
bofya hapa ujionee
Thursday, 7 May 2015
NDOA YA DIAMOND NA ZARI YAFUNGWA
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari. Diamond aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipofanya mahojiano na waandishi wetu baada ya kumuuliza kama ana mpango wa kufunga ndoa na Zari.
SIKIA MAHOJIANO HAYO
Amani: “Zari ameshakubebea ujauzito, ameshaandaa shoo ya nguvu ile ya Zari All White Party hapa kwenu Tanzania na ameonekana kukubalika na baadhi ya mashabiki wako. Je, una mpango gani wa kufunga naye ndoa sasa?
Diamond: “Khaa! Mbona kama ni ndoa na Zari nimeshafunga kimyakimya!”
Amani: “Si kweli bwana! Lini na wapi?”
Diamond: “Hapahapa Dar. Lakini siwezi kusema ni wapi kwani tulishaamua iwe kimyakimya na imepita tayari, siku chahe kabla ya ile shoo ya Mlimani City.”Amani: “Kama ni kweli kwa nini haikuwa na mashamsham kama ndoa za mastaa wengine?”
KISA CHA KIMYAKIMYA
Diamond: “Unajua bi mkubwa (mama yake mzazi, Sanura Kasim) alikuwa anaumwa, kidogo ana nafuu kwa
sasa. Ndiyo maana sikutaka mashamsham.”Amani: “Zari mwenyewe amekubaliana na uamuzi wa ndoa ya kimyakimya?”
Diamond: “Hakuwa na shida.”
KUHUSU DINI YA ZARI
Amani: “Amebadili dini? Maana ilisemekana alikuwa Muislam, akabadili kuwa Mkristo.”
Diamond: “Ilikuwa rahisi kurudi kwenye imani yake ya kwanza kwa hiyo ataendelea kuitwa Zarina.”
DIAMOND SASA
Rafiki wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini lakini wengi wanamjua, alipoulizwa kuhusu ndoa ya Diamond na Zari alisema:
“Jamani! Jamani! Jamani! Hivi kweli mnavyomjua Dangote (Diamond) nyie anaweza kufunga ndoa kwa siri au kimyakimya?”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment