Tanzania mwenyeji Kagame Cup
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
Tanzania (TFF) imekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati ngazi ya vilabu inayojulikana kama Kagame Cup.
Baraza
la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao
ndio wamiliki wa mashindano haya nahutoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki. Watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo baade mwezi huu au mapema mwezi ujao.
Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema uamuzi wa kukubali kuwa wenyeji umetolewa na shirikisho hilo mapema Jumapili baada ya kuombwa na Cecafa.
Michuano hii inatarajiwa kufanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.
Michuano hiyo inadhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame na hufanyika kila mwaka katika nchi mwanachama za ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati. Rwanda ndio ilikuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka jana inayohusisha vilabu.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars inaingia kambini Jumatatu wiki hii kwa ajili ya kuanza mazoezi ya
kujiandaa na michuano ya Cosafa itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini
baadae mwezi huu.
Mazoezi hayo pia yatakuwa ni sehemu ya
maandalizi ya kucheza michuano ya kufuzu kucheza kombe la Mataifa ya
Afrika ( AFCON) na michuano ya CHAN mwezi Juni mwaka huu.Kocha wea Stars, Mart Nooij tayari amechagua wachezaji 28 aliowaita, wapo vijana wanaochipukia na wenye uzoefu katika michuano ya kimataifa.
Nooij amesema wachezaji watakaporipoti kambini watapimwa afya zao na madakatari wa timu na kisha atachagua 20 watakaokuwa “fit” kwa ajili ya kuelekea Afrika ya Kusini.
Wachezaji watakaoingia kambini ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).
Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).
Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).
Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.
Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana.
No comments:
Post a Comment