bofya hapa ujionee

Sunday, 10 May 2015

MICHEZO-Klabu Tanzania Bara zapongezwa

Klabu Tanzania Bara zapongezwa

Manchester United itamwachia Di Maria aende PSG kwa mkopo?

Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimezipongeza klabu za Yanga, Azam na Simba kwa kumaliza katika nafasi za juu kwenye ligi kuu Tanzania bara, iliyomalizika jumamosi mei 9,2015.
Yanga ambao wameibuka mabingwa, Azam wakiwa washindi wa
pili na Simba wa tatu zipo katika mkoa wa Dar es Salaam. Kutokana na hoja hiyo, kamati ya utendaji ya DRFA chini ya mwenyekiti wake Almas Kasongo,imesema ni jambo la kufurahisha kuona timu hizo zimefanya vizuri kisoka na kuwa mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine. Ligi hiyo inahusisha timu kutoka mikoa mbalimbali.
Timu hizo zimepongezwa kutokana na matayarisho waliyoyafanya tangu kuanza kwa msimu,ambapo mabenchi ya ufundi yameonesha kuwa na nia ya dhati kuleta ushindani katika ligi.
Yanga SC na Azam Fc ndizo zitakazoiwakilisha nchi katika michuano ya vilabu barani Afrika,ambapo Yanga itakwenda huko kuwania kombe la klabu bingwa baada ya kutwaa uchampioni,huku Azam ikiwania kombe la shirikisho baada kumaliza katika nafasi ya pili, wakati Simba imemaliza katika nafasi ya tatu.

 Machester united itamwacha Dimaria  aende PSG  kwa mkopo?Manchester United itamwachia Di Maria aende PSG kwa mkopo?

Manchester United imemsajili winga wa PSV Memphis Depay kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu na huenda ikamtema mchezaji wao Angel Di Maria.
Lakini klabu ya Paris Saint-Germain ‘PSV’ ya Ufaransa imesema ipo tayari kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo kama ataruhusiwa na uongozi wa timu yake ili kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.
Mchezaji huyo alisajili kwa pauni milioni 60 akitokea Real Madrid lakini hakuonyesha kiwango kizuri msimu huu na kuwa hatarini kutemwa.
Man United awali ilitaka kumuuza mchezaji huyo lakini baadaye meneja wa timu hiyo Luis Van Gaal alibadili mawazo na kudai ataendelea kubaki kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mwingine.

No comments:

Post a Comment