WAKATI mgomo wa mabasi
ukimalizika juzi, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamekumbwa na adha
nyingine, baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kuleta madhara
mbalimbali kijamii na kiuchumi.
Katika maeneo mbalimbali ambayo waandishi wetu walitembelea leo, walikuta baadhi ya wakazi wakitoa maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao na sehemu za kufanyia bishara zao.
Katika maeneo mbalimbali ambayo waandishi wetu walitembelea leo, walikuta baadhi ya wakazi wakitoa maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao na sehemu za kufanyia bishara zao.
Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Mwanayamala
Mkwajuni maarufu kama ‘Bondeni’ wameonekana kutupia lawama Kampuni ya
ujenzi ya Strabag kuwa ujenzi wao wa barabara ndio umechangia nyumba zao
kuingiliwa na maji kwani mifereji iliyotengenezwa haikidhi uwezo wa
kusafirisha maji kwa kasi maana ni midogo, badala yake maji hujaa na
kupitisha juu kuelekea katika makazi yao.
Wakati huo huo waandishi wetu walifika
maeneo ya Jangwani na kukuta baadhi ya nyumba zilizoko bondeni zikiwa
zimezama majini, huku wakilalamika kutaka serikali iwasaidie, licha ya
ukweli kwamba walishaambiwa siku nyingi kuhama mabondeni.
Wakati huo huo, eneo la soko la Sinza-Afrika Sana, waandishi wetu waliwakuta wafanyabiashara ndogondogo wakilaumu mifereji inayopitisha maji barabarani kuziba kufuatia uchafu unaotupwa na kuziba maji kufika hadi sokoni hali inayopelekea biashara zao kudoda kutokana na wateja kukosa sehemu ya kupita.

No comments:
Post a Comment