Mnamo 13 mwezi May jenerali
mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi
amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa
rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika
jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini
Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa kuwa leo, alishindwa
kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania
Msemaji wa rais Nkurunziza Willy Nyamitwe amezungumza na mwandishi
wetu na kuthibitisha kuwa Nkurunziza aliondoka nchini Tanzania siku ya
jumatano lakini hawezi kubaini iwapo yuko nchini Burundi au la.Amesema
kuwa kutokana na maswala ya usalama hawezi kutaja mahala alipo lakini yu
buheri wa afya.20.25pm-Jenerali Godefroid Niyombare,
Shirika la habari la Reuters limenukuu baadhi ya mahojiano yaliofanywa na rais Nkurunziza na kituo cha habari cha RTNB mapema leo.
''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi'',alinukuliwa akisema.
''Nwashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.
Lakini baada ya mahojiano hayo kulikuwa na vita karibu na kituo hicho cha habari ambacho kwa sasa kimezimwa.,
Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
.
No comments:
Post a Comment